Kongamano la pili la amani Kitaifa kufanyika Dodoma Julai 13

By Ibrahim Joseph , Nipashe
Published at 07:30 PM Jul 11 2025
Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa la Taifa, Sheikh Ali Hamisi Ngeruko.
Picha:Ibrahim Joseph
Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa la Taifa, Sheikh Ali Hamisi Ngeruko.

Kongamano la pili la Amani Kitaifa linatarajiwa kufanyika Julai 13, 2025 mkoani Dodoma, likihusisha viongozi mbalimbali wa dini kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 11, 2025 jijini Dodoma, Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa la Taifa, Sheikh Ali Hamisi Ngeruko, amesema lengo kuu la kongamano hilo ni kujadili masuala ya amani ya taifa.

Sheikh Ngeruko ameeleza kuwa kongamano hilo litajadili mada mbalimbali ikiwemo athari za mitandao ya kijamii katika kuchangia kuvuruga amani, afya ya akili, mchango wa vyombo vya dola na taasisi za dini katika kulinda amani, pamoja na umuhimu wa vyombo vya habari katika kudumisha amani.

Aidha, amebainisha kuwa kongamano hilo ni sehemu ya mwendelezo wa makongamano ya amani yanayoandaliwa na viongozi wa dini nchini, ambapo kongamano la kwanza lilifanyika jijini Dar es Salaam.