MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imesema inatarajia kuanzisha kanzidata yenye taarifa mbalimbali kuhusu urithi wa asili, ikiwamo idadi ya wanayama wanaopatikana hifadhi hiyo.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Uhifadhi NCAA, Abdul-Razaq Badru wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea.
Amesema Hifafhi ya Ngorongoro ni sehemu yenye urithi usiosahaulika, kutokana na kuwa eneo la binadamu wa mwanzo, ambaye alikuwa na mwili mkubwa.
"Pamoja na mambo yote, Ngorongoro inafahamika kwamba mi chanzo cha maisha ya binadamu wa mwanzo aliyepata kufahamika, kwa hiyo tunakaribisha watu waje wamuone, siyo binadamu kama sisi ni mwenye upekee na maajabu yake, yote hayo ni katika mazao yatakayotengenezwa kufanya wakajua historia ya maisha binadamu.
"Binadamu na wanyama na mazingira na pia wanyama wasiopatikana sehemu nyingi katika Afrika na Tanzania na wenyewe wataongezwa kwa idadi katika hifadhi yetu."
Amesema wanaendelea kutengeneza zaidi uhifadhi katima hifadhi hiyo, ili uweze kuainishwa kwenye mahitaji yanayokuja, uhifadhi.
"Kwa maana ya wanyamapori, kuboresha na kuhakikisha mazingira yanazidi kutunzwa na ule uoto wa asili unazidi kutunzwa, ili kufanya Ngorongoro iendelee kubaki na upekee wake na kuendelea kukidhi madhumuni yake ya kuwa sehemu yenye uhifadhi wa viumbe asili wa wanyamapori unaowezesha wanadamu na viumbe wengine kuishi."
Kadhalika, amesema wana mpango wa kutanua wigo wa mazao ya vivutio katika hifadhi hiyo ukiacha yale yaliyozoeleka.
"Yako mambo mengi sana tunayofanya kama Ngorongoro mojawapo ni kutanua wigo wa mazao yaliyopo na hivi karibuni tutazindua mazao mbalimbali kutoka katika yale mazao yanayofahamika.
"Tutakuwa na mazao mengi ambayo yanatokana na upekee, mfano pale pana creater, wanyama, maji na pana mimea ya aina mbalimbali ambayo watu hawaifahamu, kwa kushirikiana na wenzetu katika sekta yetu ya utalii tutatengeneza mazao ya aina ile."
"Lakini pia tutaboresha huduma za mle ndani za watu wanaokuja kutembelea huduma za malazi, chakula, ili mtu anapokuja kutembelea, aweze inanufaika."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED