Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango,amesema bara la Afrika kwa mwaka mmoja linakaridiwa kuhitaji fedha za utekelezaji wa mbiundombinu mbalimbali kiasi cha Dola za Kimarekeni Bilioni 130 hadi 170 kwa ajili ya kufikisha huduma muhimu kwa wananchi.
Dk.Mpango,alisema endapo imetokea fedha hizo,zimekosekana uchangia kurudisha nyuma ukuaji wa uchumi na kupunguza ufikiwaaji wa huduma muhimu kwa wananchi kwenye nchi za bara la Afrika.
Alisema hayo jana jijini Arusha,wakati akifungua Mkutano wa 14 kwa Watengeneza Sera ya Ulinzi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii Afrika(ASSA).
Pia alisema pengo la ufadhili wa miundombinu kwa mwaka inakadiriwa kuwa ni kati ya Dola za Kimarekani Bilioni 68 mpaka 108 kwa kuzingatia uimarishaji wa dunia pamoja na ufadhili kwa wawekezaji.
Alisema wachambuzi wa maendeleo wanakubaliana kuwa usalama wa fedha za mifuko ya kijamii zimewekwa zaidi kama kichocheo cha kuharakisha maendeleo ya miundombinu.
Hata hivyo,amewataka watunga sera za kinga ya mifuko hiyo ya kijamii za Afrika, wanaoshiriki katika nkutano wa kuja na maoni na suluhisho ya vitendo juu ya jinsi usalama wa mifuko hiyo.
“Ninawapongeza waandaaji wa mkutano huu kwa juhudi za kuuandaa,pia kuchagua mada hii muhimu sana kwa kuwa mazingira ya ulimwengu ya maendeleo ya ufadhili yamezidi kuwa magumu kwa sababu ya migogoro ya jiografia na nafasi finyu ya kifedha kwa nchi nyingi za Kiafrika.Kama nyinyi nyote mnavyoju kuwa maendeleo ya miundombinu iko kwenye moyo wa Ajenda ya Bara letu 2063:
Pia alisema Afrika inatarajia kubadilisha miundombinu ili kuiboresha na kuunganishwa kupitia reli zenye kasi kubwa, barabara kuu na miundombinu ya nguvu ya ICT.
Licha ya kuzungumza hayo,alisema bara la Afrika linahitaji usalama wa nishati kupitia mabwawa ya nguvu ya kikanda,safi na ya bei nafuu za nishati sambamba na kuongeza muunganisho wa kidijiti kwa kujenga miundombinu ya ICT,uchumi wa dijiti na uvumbuzi ili kuleta ushindani duniani.
Aidha alisem ulinzi wa mifuko ya kijamii na miundombinu Maendeleo yana uhusiano wa mfano kwa kuwa kuboresha maisha kupitia uundaji wa kazi na kuchochea uchumi shughuli,hivyo kupunguza hitaji la mipango ya Usalama wa Jamii.
Alisema usalama wa miradi ya mifuko ya kijamii yenye nguvu huleta mchango katika kijamii kwa kuruhusu watu zaidi kushiriki katika shughuli za kiuchumi zenye tija,kuboresha maisha ya wananchi na ustawi,hivyo kupunguza umaskini na kuleta usawa wa kuwa na miundombinu nzuri.
Makamu wa Rais,alisema kwa Tanzania,fedha za mifuko ya kijami zimesaidia kuongeza nguvu katika jitihada serikali kwa miaka katika kujenga miundombinu ikiwamo kutekeleza miradi ya maeneo ya makazi na biashara ya makazi.
Vilevile alisema makadirio mengine yaliyofanyika yanaonyesha kuwa sekta isiyokuwa rasmi barani Afrika inachukua asilimia 40 hadi 60 ya uchumi kwenye maendeleo ya miundombinu yhususani katika sekta ya vijijini.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,(Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Ridhiwani Kikwete,alisema mkutano huo,utafanya mapitio ya sera na kufanya maboresho kwa dhana ya kukuza uchumi wa bara la Afrika.
Alisema kupitia mkutano huo,watazungumzia masuala kuweka mpango mkakati wa usalama wa mifuko hiyo ili iwe kichocheo cha maendeleo ya miundombinu na ukuaji wa uchumi wa jamii.
Katibu Mkuu wa ASSA, Meshach Bandawe,alisema katik mkutano watasikiliza changamoto na kubadilishana uzoefu wa mambo gani yanayopaswa kufanyiwa kazi ili kuhakikisha suala la utekelezaji wa miundombinu kwa mifuko hiyo linakuwa endelevu kwa ukuaji wa uchumi.
Kadhalika alisema washiriki wa mkutano huo,wametoka nchi 15 ikiwamo Tanzania ambaye ni nchi mwenyeji,Kenya,Uganda,Zambia,Zimbabwe,Sierra Leone,Rwanda, Burundi,Malawi,Komoro,Sudani Kusini,Namibia, Covid,Ghana, Afrika Kusini,DRC Kongo na Nigeria pamoja na wajumbe wanaowakilisha washirika wao wa kimataifa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED