TANZANIA imeingiza miradi 90 kwenye mabingwa wa tuzo za za kimataifa zenye heshima kubwa katika uwanja wa teknolojia ya habari na mawasiliano (World Summit on the Information Society -WSIS Prizes 2025) ambazo huandaliwa na Shirika la WSIS.
Hatua hiyo ni kusherehehea mafanikio makubwa katika
Anga la kimataifa ya teknolojia.
Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Mei 25,2025 na imeeleza kuwa mchakato mkali wa Tuzo za WSIS 2025, ambao ulishuhudia miradi 973 ikiwasilishwa na 360 kuchaguliwa kupigiwa kura na Tanzania kuibuka kinara.
“Kwa fahari kubwa, kati ya miradi hiyo 90, miradi 23 inatoka barani Afrika, ikiwakilisha nchi 20 tofauti. Jambo la kujivunia zaidi, miradi mitatu toka Tanzania imefanikiwa kufikia hatua ya Ubingwa (Champions),”imefafanua taarifa hiyo.
Aidha, hatua hiyo inaiweka Tanzania katika nafasi ya kipekee kama nchi yenye idadi kubwa zaidi ya miradi ya kibingwa katika vipengele ya matumizi ya TEHAMA, ambayo inajumuisha manufaa katika nyanja zote za maisha, ikiwemo afya mtandao (e-health), serikali mtandao (e-government), na sayansi mtandao (e-science).
Miradi mitatu kutoka Tanzania ni pamoja na mfumo wa eMrejesho V2 kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mradi wa huduma za Afya Zanzibar kutoka Pharmacess na STEM4All kutoka Chuo kikuu cha Mt. Joseph.
“Mafanikio haya yanadhihirisha jitihada na ubunifu mkubwa na usimamizi madhubuti wa Sera za kidigiti za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan katika kutumia teknolojia kuleta mabadiliko chanya,”amesema.
Macho na masikio sasa yatakuwa Geneva, Uswisi, ambapo washindi 18 wa mwisho watatangazwa rasmi kwenye tukio la mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Habari (WSIS+20) mnamo Jumatatu, Julai 7, 2025.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED