Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), imesema kuwa wanaandika vitabu vya kiada na kwamba madai kwamba wanaandikiwa si ya kweli
Aidha,imesema ili kitabu kiwe bora wanaelezwa waanzie wapi na waishie wapi, na kwamba wa nasisitizwa ushirikiano na wataalamu wengi ili kupata ubora.
Ufafanuzi huo umetolewa na Mkurugenzi wa TET,Dk.Aneth Komba wakati akizungumza na wahariri kuhusu miaka 50 ya taasisi hiyo kwa kauli mbiu ya Kitabu Kimoja Mwanafunzi Mmoja na #MpeKitabuGusaNdoto
Kuhusu kuandika vitabu,amesema wanaandika kwa kufuata miongozo na taratibu zao,na kwamba katika kuandaa mitaala wanashirikisha wadau kuanzia kuandaa hadi kutekeleza.
Aidha, amesema walimu walishirikishwa kwenye uandaaji wa mitaala iliyoboreshwa ya 2023 na walimu wote walipewa mafunzo,na ambao hawajapata mafunzo wanafikiwa kwa utaritibu wa mafunzo endelevu.
Amesema vitabu vingi na kwa mwaka huu wa fedha wamechapisha vitabu mil 9,na kwamba wakishakamilisha vitabu wanaalika wazabuni ambao wanapata kandarasi wanakwenda kuchapa na kwamba huenda wanachapisha kokote.
"TET tunachapisha vichache lakini vingine tunawapa wakandarasi wanakwenda kuchapisha wanakokojua wenyewe sisi tunachoangalia ni ubora wa kazi tuliyompa,"amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED