Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), imesema inatarajia kujenga kiwanda kikubwa cha uchapaji ili kupunguza gharama, kuongeza mapato taasisi na kuharakisha upatikanaji wa vitabu nchini.
Hayo yamesema na Mkurugenzi wa TET,Dk.Aneth Komba wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari leo Juni 13,2025 kuhusu kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya TET yatakayofanyika Juni 17,mwaka huu.
Amesema lengo ni kuimarisha ushirikiano baina ya TET na taasisi na mashirika ya ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuendelea kuweka mazingira rafiki katika uboreshaji wa elimu nchini pamoja na kujifunza kutoka kwa nchi nyingine.
Dk. amesema mgeni rasmi ni Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa ambaye atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwa kauli mbiu ya kitabu kimoja mwanafunzi mmoja,na #MpeKitabuGusaNdoto.
Amesema shughuli zitakazofanyika siku hiyo ni uzinduzi wa Soma Kwanza TV,mfumo wa usimamizi wa kujifunzia (MEWAKA).
Nyingine ni uzinduzi wa jalada la kitabu cha hadithi za watoto Soma na Wajukuu, na kupokea kitabu chenye orodha ya wachangiaji na kitabu cha miaka 50 ya TET.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED