Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), imesema inatarajia kusambaza kopyuta mpakato 16,819 katika mikoa 10 nchini.
Akizungunza na wahariri na waandishi wa habari kuhusu kilele cha miaka 50 ya maadhimisho ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kitakachofanyika Juni 17,2025 na mgeni ni Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,Mkurugenzi wa TET, Dk.Aneth Komba amesema lengo ni kukuza elimu kwa kutumia digital.
Amesema mikoa hiyo saba ni kutoka Tanzania Bara na mitatu kutoka Zanzibar na ni kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
"Tumeanza kusambaza kopyuta katika shule 10 nchini ili kupunguza matumizi ya vitabu halisi kwasababu ni gharama sana kuchapisha vitabu,matokeo tutakayoyaona yatatuwezesha kusambaza vitabu kidigitali,"amesema Dk.Komba.
Aidha, TET ina Soma Kwanza TV ambayo inafikisha elimu kwa wanafunzi wa ngazi mbalimbali nchini,majukwaa ya TEHAMA na kutumia fursa zilizopo kwenye digital kufikia walimu na wanafunzi wengi.
Aidha,amewataka wazazi kuwapa watoto wao fursa za kutumia vifaa vya digitali,ili wajifunze teknolojia na kwamba wazazi wafuatilie kwa karibu shughuli wanazofanya watoto wao mtandaoni ili wasiwe na natumizi mabaya.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED