Waziri Mkuu azindua Albino Mobile App

By Renatha Msungu , Nipashe
Published at 01:30 PM Jun 14 2025
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira Vijana na wenye Ulemavu,Ridhiwani Kikwete,wakati wa uzinduzi  Mobile App ya kusajili na kukusanya taarifa za watu wa kundi hilo
PICHA: RENATHA MSUNGU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira Vijana na wenye Ulemavu,Ridhiwani Kikwete,wakati wa uzinduzi Mobile App ya kusajili na kukusanya taarifa za watu wa kundi hilo

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amezindua 'Albino Mobile App' ambayo ni program ya simu janja itakayowezasha usajili na ukusanyaji wa taarifa za watu wenye Ualbino na wenye Ulemavu kwa njia ya kidigitali.

Aidha, amesema Mfumo wa Albino Mobile App ni sehemu ya Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Watu wenye Ulemavu (PD – MIS) utaongeza ujumuishaji wa Watu wenye Ulemavu kwenye huduna za kijamii na maendeleo.

Amesema hayo leo Juni 13, 2025 wakatu alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimiwho ya Siku ya Kimatqifa yw kukuza uelewa kuhusu Ualbino ambayo yamefanyika katika uwanja wa Mwanga Center, mkoani Kigoma. 

Vile vile, amewaagiza Wakuu wa Mikoa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi kwa Watu wenye Ualbino, Mkakati wa Taifa wa Teknolojia Saidizi na Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Taarifa za Watu wenye Ulemavu (PD-MIS) katika ngazi ya Halmashauri.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi Vijana, Ajira na Wenye UlemavuRidhiwani Kikwete amesema kuwa programu hiyo janja ya ' Albino Mobile App' itarahisisha na itahakikisha usahihi wa taaarifa za usajili wa watu wenye Ualbino katika maeneo mbalimbali nchini.

“Mfumo huu utapunguza gharama za usafiri na usafirishaji wa vifaa kwa ajili ya usajili, na pia kuwezesha upatikanaji wa takwimu sahihi zinazosaidia Serikali kupanga na kutekeleza sera kwa ufanisi” amesema

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS), Godson Mollel amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeendela kuwafanyia mambo makubwa watu wenye Albino nchini ikiwemo kutenga fedha kwa ajili ya kuwezesha upatianaji wa mafuta kinga ambayo hugawiwa bure.