SERIKALI wilayani Mkalama mkoani Singida imewakabidhi wazee 20 kadi za msamaha wa matibabu bure wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili kwa Wazee Duniani zilizofanyika kimkoa wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali, akikabidhi kadi hizo leo (Juni 15,2025) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, aliwataka wazee kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa kusimamia maadili na malezi bora ya watoto pamoja na kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili ndani ya familia na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Mkoa wa Singida, Mchungaji Mbura Joel, alitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zinazofanyika katika kulinda haki na ustawi wa wazee nchini.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED