Tanzania, India kushirikiana kuinua sekta za habari, filamu na burudani

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:49 PM May 03 2025
news
Wizara ya Habari
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza na Waziri wa Nchi, Wizara ya Habari na Utangazaji wa India, Dk. Roganathan Murugan.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, ameeleza kuwa mkutano wa kwanza wa kimataifa wa masuala ya habari, filamu na burudani (World Audiovisual & Entertainment Summit-WAVES) unaoendelea katika jiji la Mumbai nchini India, umeifungulia Tanzania fursa katika kuendeleza sekta za habari, filamu na burudani.

Prof. Kabudi ameeleza fursa hizo leo Mei 3, 2025 mara baada ya kufanya kikao cha pembezoni (side meeting) na Waziri wa Nchi, Wizara ya Habari na Utangazaji wa India, Dk. Roganathan Murugan.

Aidha, katika mazungumzo, mawaziri hao wamekubaliana kufufua upya kwa Idhaa ya Kiswahili ya Shirikia la Utangazaji la India la All India Radio kwa kushirkiana na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), ili kukifanya Kiswahili kitangazwe na Radio hiyo ya India na kukifanya kisikike tena katika Bara Hindi na sehemu zingine duniani ambako All Radio India inasikika.

 

“Pmoja na hayo tumekubaliana tena kuanza kuwa na ushirikiano wa kiufundi na All Radio India hasa katika mitambo mipya ya mipya utangazaji radio ya kidigitali ya DRM 30+ ambapo India wenzetu wa India wapo mbali sana, tumeweza kutembelea maonesho na tumeona jinsi gani India wamekwenda mbali sana katika teknolojia ya utangazaji na urushaji wa matangazo,” ameeleza Prof. Kabudi.

 

Waziri Kabudi ametaja maeneo mengine ya ushirikiano kuwa ni katika eneo la utengenezaji wa filamu na kuangalia jinsi gani Tanzania na India zinaweza kushirikiana katika kutengeneza filamu, maudhui ya filamu na kuzisambaza filamu za Tanzania nchini India na za India kuendelea kununuliwa na kutumiwa nchini Tanzania.

 

Aidha, amesema eneo lingine ambalo Tanzania inahitaji kulitumia ili kuhakikisha soko lake la filamu linasambaa nchini India ni pamoja na kuweka maneno ya tafsiri ya Kihindi na Gujirati kwenye filamu zinazotengenezwa Tanzania, ili ziweze kuuzika nchini India na pia kuangalia taasisi mpya ya India inajihusisha na sanaa bunifu itakavyoweza kuchukua wanafunzi kutoka Tanzania.

 

“Chuo hicho ni kipya na kinasisitiza matumizi ya teknolojia kuendana na mazingira ya nchini ambazo zinahitaji teknolojia hiyo”, amesisitiza Prof. Kabudi huku akionesha umuhimu kwa wasanii wa Tanzania kutumia fursa hiyo ya mafunzo na tafiti katika kimarisha na kuboresha kazi za sanaa.

 

Aidha, Prof. Kabudi amemueleza Waziri wa Habari na Utangazaji wa India, Dk. Murugan juu ya uzuri wa Tanzania na kumueleza kuwa Tanzania inawakaribisha watengeneza filamu kutoka India kutumia maeneo ya kimkakati nchini kama Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro. 

Pia amesema Zanzibar na maeneo mengine kuyatumia kurekodi filamu za kihindi na kuwaalika watu mashuhuri wa India wakiwemo waigizaji na watengeneza filamu kuja kutembekea Tanzania na kuona maeneo watakayoshirikiana na Bodi ya Filamu Tanznaia.

 

“Tumewakaribisha katika maonesho yetu ya filamu ya kila mwaka kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF) na Sinema Zetu, na wao pia wametualika katika maonesho yao ya sinema ambayo mara nyingi yanafanyika mwishoni mwa mwezi Novemba,” amesisitiza Waziri Kabudi.

 

Mbali na kushiriki mkutano na kuoata fursa ya kufanya mazungumzo na Waziri wa Habari na Utangazaji wa India, Kabadi na ujumbe wake kutoka Tanzania walipata fursa ya kutembekea maonesho yanayoendana na mkutano huo pamoja na kwenda kujionea eneo maarufu Bollywood (Film City), ambalo hutumika kutengenza filamu nyingi za kihindi na kujifunza mambo mengi yatakayosaidia kwenye ujenzi yatakayosaidia wakati wa ujenzi wa Arts and Sports Arena