VIONGOZI wa kisiasa, dini na serikali jana waliungana na mamia ya wananchi mkoani Tanga kumzika aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu (82),katika eneo la maziko ya familia Paje, huku akitaja alama alizoacha nchini.
Akizungumza kwenye mazishi yaliyofanyika Machi 30,2025 Naibu waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Hamisi Mwijuma alimaarufa Mwana FA amesema wengi walikuwa wakiingia kwenye siasa na shughuli za utumishi serikali walikuwa wakimuangaliamzee huyo kama nembo ya mkoa wa Tanga
Alisema kwa sababu watu wengi wamejifunza mambo mengi kutokana na yeye kutokana na yeye sio kwa anayoyasema hata anayokuuliza na hivyo walikuwa wakijifunza mambo mengi sana kupitia yeye .Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Januari Makamba amesema Balozi Mwapachu alikuwa ni rafiki wa wengi na aligusa maisha ya watu wengi na alisaidia na alikuwa na muda kwa kila mtu ametimiza wajibu kwa bara la afrika ,kwa nchi yake na watu wa Tanga hivyo wanamuomba mwenyezi mungu amuepushe na adhabu ya kaburi amjalie pepo.
“Nitamkosa mzee ucheshi wake mafunzo yake busara zake natoa pole kwa wafiwa wote”alisema
Akizungumza kwa niaba ya Familia ya Mzee Mwinyi amesema walikuwa na mashirikiano na wanakubaliana kwa kila jambo pale ambapo jambo linatokea hivyo wanaomboleza na wanasherehekea maisha ya mzee huyo ameandika hadithi njema ameishi vizuri kwenye jami na mafanikio mazuri nambo yake na mahusiano na watu ni mazuri
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian amesema msiba huo umemgusa sana Rais Samia Suluhu kutokana na mchango wa marehemu katika nyadhifa mbalimbali.
Amesema pia hekima zake kuacha elimu kubwa vizazi vitajifunza na katika harakati za uhuru kwa sababu ya mchango wao mkubwa katika ukombozi wa nchi wao kama Tanga walipata heshima kubwa kwa familia hiyo kupata watu ambao walikuwa wanatoa mchango wao mkubwa katika nyadhifa mbalimbali serikali.
Kiongozi Mkuu Mstaafu wa Chama cha ACT Wazaendo, Zitto Kabwe amesema Mwapachu alikuwa Mtanzania mwanazuoni aliyechangia wananchi kukua kimawazo na kifikra.
Naye, Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Afrika Mashariki anayeshughulikiamasuala ya Afrika Mashariki,Steven Mbundi ameacha alama kubwa kwenye EAC.
Katibu huyo ambaye alimwakilisha Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema Mwapachu ni Katibu wa tatu wa EAC aliyefanya shughuli nyingi za maendeleo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED