Ajali yaua wanakwaya sita wa KKKT, majeruhi 73

By Godfrey Mushi , Nipashe Jumapili
Published at 04:22 PM Mar 30 2025
Mkuu wa Wilaya hiyo, Kasilda Mgeni
Picha: Mtandao
Mkuu wa Wilaya hiyo, Kasilda Mgeni

WANAKWAYA sita wa Usharika wa Chome wa Dayosisi ya Pare ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), wamepoteza maisha katika ajali ya barabarani, wakati wakienda kwenye huduma ya uimbaji Usharika wa Vudee, Wilayani humo.

Mbali na wanakwaya hao, abiria mmoja amefariki dunia papo hapo, baada ya basi la abiria, mali ya Kampuni ya Osaka, kuacha njia na kupinduka katika eneo la Njoro, Wilayani Same.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Kasilda Mgeni, amethibitisha ajali hizo mbili kusababisha vifo saba Machi, 30 mwaka huu, huku akieleza zimeacha majeruhi 75.

Kwa habari zaidi tembelea epaper.ipp.com