'MBALI NA KUKATIKA UMEME ,TUNAONGEA NA UMMA'

By Halima Ikunji , Nipashe Jumapili
Published at 06:24 PM Mar 30 2025
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limetambuliwa kuwa moja kati ya taasisi za umma zilizofanya vizuri katika kuhabarisha umma, kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu huduma zao, ikiwamo kukatika kwa umeme na kutunukiwa tuzo nne
Picha: Mtandao
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limetambuliwa kuwa moja kati ya taasisi za umma zilizofanya vizuri katika kuhabarisha umma, kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu huduma zao, ikiwamo kukatika kwa umeme na kutunukiwa tuzo nne

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limetambuliwa kuwa moja kati ya taasisi za umma zilizofanya vizuri katika kuhabarisha umma, kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu huduma zao, ikiwamo kukatika kwa umeme na kutunukiwa tuzo nne.

Tuzo hizo zimetolewa jana, jijini Dar es Salaam na Chama cha Maofisa Uhusiano na Mawasiliano Tanzania (PRST).   

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hizo, Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Irene Gowelle, amesema ni nafasi nzuri kwa shirika hilo na kwamba wadau wametambua uzito wa kile wanachokifanya katika sekta ya mawasiliano.

“Kwa kuzingatia changamoto mbalimbali zinazoikumba huduma yetu, ikiwamo kukatika kwa umeme lakini sisi kama kitengo cha mawasiliano hiyo haikuwa sababu ya kutufanya tushindwe kuufahamisha umma kwa wakati” amesema Irene

Aidha amewashukuru waandaaji wa tuzo hizo akisifu zinawapa hamasa na furaha kwa kuwa lipo kundi limetambua kazi nzuri wanayoifanya.

Katibu wa PRST, Ndege MaKula aliwashukuru washiriki wote walioshinda na walioshindwa, huku akiwataka kujipanga vizuri na kuandaa kazi bora, ili mwakani kushinda.