WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema wizara hiyo itachangia uboreshaji wa miundombinu ya elimu katika Shule ya Msingi Pangani iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kibaha.
Prof. Mkenda ameyasema hayo aliposhiriki mbio za Coast City Marathon zilizofanyika Kibaha ambazo zilikuwa na lengo la kuchangia fedha kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu katika Shule ya Msingi Pangani.
Amesema wizara yake itaangalia namna ya kuchangia kuungankono jitihada zilizofanywa na waandaaji wa mbio za Coast City Marathon.
Kadhalika waziri huyo amesema yuko tayari kushiki kwa wakati mwingine waandaaji watakapo mkaribisha kuchangia mambo ya maendeleo kama wanavyofanya sasa.
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Rashid Mchatta amemshukuru waziri huyo kwa kutenga muda wake na kushiriki katika mbio hizo.
Mwenyekiti wa waandaaji wa mbio hizo Dk. Frank Muhamba amesema kila mwaka wamekuwa wakiandaa na kufanya mbio hizo ambazo mbali ya kuchangia mambo ya kijamii pia wamekuwa wakitoa zawadi mbalimbali kwa washindi wa km 5, 10 na 21.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED