Nikiwa na simu yangu niko na PSSSF-Mwanachama

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:31 PM Jun 05 2025
Hawa Hamad
Picha: Mpigapicha Wetu
Hawa Hamad

“Nikiwa na simu yangu niko na PSSSF,” hayo ni maneno ya mwanachama wa PSSSF, Hawa Hamad wa jijini Tanga muda mfupi baada ya kujiunga na PSSSF Kidijitali na kuanza kujihudumia yeye mwenyewe.

Hawa mbaye ni mtumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) jijini Tanga, ameyasema hayo jana Juni 4, 2025 kwenye maonesho ya 12 ya biashara na utalii Tanga, yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako.

Maofisa wa PSSSF wamefanya huduma ya kutembelea banda kwa banda kujua changamoto zao, kutoa huduma mbalimbali na kutoa elimu ya Mfuko  “PSSSF Banda kwa banda” lengo ikiwa ni kuwafikishia huduma wanachama wake kwenye maonesho mbalimbali yanayozikutanisha taasisi za umma na wananchi.

Mwanachama mwingine aliyefurahishwa na huduma ya PSSSF kidijitali baada ya kujiunga ni Rutta Kihama, amesema kupitia PSSSF Kidijitali ofisi imehamia mkononi mwake.