Hukumu ya P Diddy kusomwa kesho Brooklyn

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:45 PM Oct 02 2025
Sean Combs ‘P Diddy.
Picha: Mtandao
Sean Combs ‘P Diddy.

Nyota wa hip hop na mfanyabiashara mashuhuri Sean Combs ‘P Diddy’ anatarajiwa kusomewa hukumu yake kesho mjini Brooklyn, Marekani, baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya kusafirisha watu kwa ajili ya ukahaba.

Diddy amekuwa akishikiliwa katika Metropolitan Detention Center (MDC) kwa mwaka mmoja sasa, akikabiliwa pia na tuhuma za njama za kihalifu na unyanyasaji wa kijinsia, ingawa amekanusha mashitaka hayo.

Jopo la majaji lililokaa Julai 2025 lilimkuta na hatia kwenye makosa mawili, hali iliyozua maoni mseto duniani—wapo walioshangazwa, huku wengine wakiona ni ushindi wa haki kwa waathirika.

Kesho dunia itasubiri kuona kama mahakama itampa adhabu kali kama wanavyotaka waendesha mashtaka, au nafuu kama wanavyodai mawakili wake kwa hoja kwamba tayari amekaa gerezani kwa mwaka mmoja akisubiri hukumu.