Vikundi 24 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida vimenufaika na mikopo yenye thamani ya Sh milioni 236.3, fedha ambazo zinatokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri kama ilivyoelekezwa na serikali.
Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi fedha hizo, Meya wa Manispaa ya Singida, Geofrey Mdama, amesema lengo la utoaji wa mikopo hiyo ni sehemu ya mpango wa halmashauri kuhakikisha makundi maalum yanawezeshwa kiuchumi, kupatiwa mtaji, na kujengewa uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Joanfaith Kataraia, amesema katika kipindi cha Julai hadi Disemba 2025 Halmashauri ya Manispaa ya Singida imeshatoa jumla ya mikopo ya Sh. bilioni 1.058 kwa vikundi 78 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Ametoa mchanganuo kuwa kai ya vikundi hivyo 78, vikundi 57 vya wanawake vimekomeshwa Sh.milioni 722.365, vijana vikundi 17 zimekopeshwa Sh.milioni 323.100 wakati vikundi vinne vya watu wenye ulemavu vimekopesha Sh.milioni 13.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED