Mashabiki wa soka nchini wamepatiwa unafuu wa usafiri kuelekea Morocco kuishangilia timu ya taifa, Taifa Stars, inayotarajiwa kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zinazoanza Desemba 21 mwaka huu. Hatua hiyo imeratibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na kampuni ya usafirishaji ya Blueberry Travels.
Akizungumza kwa niaba ya BMT, Benson Chacha amesema mpango huo umeanzishwa baada ya mashabiki wengi kupiga simu na kutuma ujumbe kuulizia namna ya kusafiri kwa pamoja kwenda Morocco.
“Kumekuwa na mwitikio mkubwa wa mashabiki kutaka kujua jinsi ya kusafiri. Ndiyo maana BMT na TFF tukatafuta kampuni itakayorahisisha safari, na tumepata Blueberry Travels ili kuwawezesha mashabiki wengi kwenda kuipa sapoti Taifa Stars,” amesema Chacha.
Kwa upande wake, Ofisa Masoko wa Blueberry Travels, Kelvin Charles, ameishukuru TFF na BMT kwa kuwapa nafasi hiyo, akibainisha kuwa wameandaa vifurushi rafiki kwa kuzingatia vipato vya Watanzania. Vifurushi hivyo vinajumuisha nauli ya kwenda na kurudi, malazi na usafiri wa ndani nchini Morocco.
Kwa mujibu wa Charles, gharama za vifurushi ni kama ifuatavyo:
Kwa upande wa maandalizi ya timu, Ofisa Habari wa TFF, Cliford Mario Ndimbo, amesema kikosi kinaendelea vizuri na maandalizi, huku morali ya wachezaji ikiwa juu.
“Wachezaji waliokuwa nje ya nchi wanaendelea kuripoti kambini kujiunga na wenzao. Malengo makubwa ni kufika hatua ya mtoano, ambayo itatupa nafasi nzuri ya kusonga hadi robo fainali,” amesema Ndimbo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED