Manispaa ya Kibaha yamkabidhi mwenye ulemavu baiskeli

By Julieth Mkireri , Nipashe
Published at 01:14 PM Dec 12 2025
Manispaa ya Kibaha yamkabidhi mwenye ulemavu baiskeli.
Picha: Mpigapicha Wetu
Manispaa ya Kibaha yamkabidhi mwenye ulemavu baiskeli.

Manispaa ya Kibaha imemkabidhi baiskeli kijana mwenye Ulemavu Goodluck Mchome, mkazi wa Kata ya Kibaha Mwendapole, anayesoma Darasa la ili Shule ya Msingi Tumbi.

Baiskeli hiyo ni kwa ajili ya kumsaidia kufika shuleni kwa urahisi pamoja na kutekeleza majukumu yake ya kila siku awapo maeneo ya nje na ndani ya nyumbani.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha ambapo Mkurugenzi Dk. Rogers Shemwelekwa, amemkabidhi alikabidhi baiskeli hiyo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Dk. Shemwelekwa amesema Serikali itaendelea kufuatilia hali ya mwanafunzi huyo na kuhakikisha chombo hicho kinafanya kazi muda wote kumuwezesha kufika shule.

“Tutaendelea kuhakikisha baiskeli hii inakuwa katika hali nzuri, ikiharibika muda wowote, tutaitengeneza ili Goodlack anaendelea kupata elimu bila kikwazo chochote,” amesema Dk. Shemwelekwa.

Kwa upande wake, mama mzazi wa kijana huyo, Jaqueline Mbwambo, ameishukuru Manispaa ya Kibaha, kwa msaada huo akisema imeondoa changamoto  ya usafiri iliyokuwa ikimkabili mwanawe.

“Namshukuru sana Rais Samia na Manispaa ya Kibaha kwa kutatua changamoto ya usafiri iliyokuwa ikimzuia mwanangu kwenda shule kwa wakati. sasa ataweza kusoma kwa amani na kufikia ndoto zake,” amesema mama huyo.

Hatua hiyo ni jitihada za Manispaa ya Kibaha katika kujali na kuboresha maisha ya watu wenye mahitaji maalum na kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma katika kupata elimu.

IMG-20251211-WA0067.jpg 140.02 KB