Siku chache baada ya kusambaa kwa video inayowaonyesha kuwa Diamond na Zuchu wamefunga ndoa, mama mzazi wa Zuchu, Khadija Kopa, amekataa kuzungumzia ndoa hiyo.
Nipashe Digital ilimpigia simu malkia huyo wa mipasho na kusalimiana naye, kisha kumuuliza swali kuhusu ndoa hiyo kama anaijua au ametoa baraka zake kama mzazi wa binti huyo.
Hata hivyo, badala ya kujibu, msanii huyo alikata simu na hata alipotafutwa, hakupokea, kitendo kilichoonyesha hakuwa tayari kuzungumzia ndoa ya wawili hao.
Hata alipopigiwa, hakupokea na kuamua kuwa kimya, kitendo kilichoonyesha kwamba hakuwa tayari kuzungumzia ndoa ya binti yake ambayo sasa ni gumzo kwenye mitandao ya kijamii.
Msanii Naseeb Abdul au Diamond Platnumz na mpenzi wake Zuhura Othman 'Zuchu', walitangaza kufunga ndoa. Lakini ujumbe wa Diamond juu ya ndoa hiyo, unaonekana kuwachanganya wengi.
Mchanganyo huo unatokana na kuwapo kwa taarifa kuwa wawili hao walishaachana muda mrefu, huku madai hayo yakitofautiana na ujumbe wa mama wa Diamond, kupitia Instagram yake, alithibitisha ndoa hiyo.
Ingawa ndoa hiyo imekuwa ya siri, watu mbalimbali mitandaoni wamejitokeza kuwapa hongera, huku wengine wakiwa hawana uhakika kama wawili hao wamefunga ndoa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED