MWIGIZAJI maarufu na nyota wa Hollywood, Angelina Jolie, ameamua kutalikiana na mumewe Brad Pitt, baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka 10.
Wakili wake ameviambia vyombo vya habari. Hapakuwa na maoni ya mara moja kutoka kwa wakili wa Pitt.
Wawili hao walifunga ndoa mwaka wa 2014 na wana watoto sita, wakiwamo waliowasili.
Wawili hao waliingia katika malumbano makali ya kulea mtoto katika miezi iliyofuata tangazo la talaka lilitoka.
Mwaka 2021 hakimu alitoa haki ya pamoja ya malezi ya watoto kwa wazazi wote wawili.
Wanandoa hao walijulikana kama ‘Brangelina’ kwa maana ya kifupi cha majina yao.
Waliigiza pamoja kwenye filamu ya 2005 ‘Mr and Mrs Smith’.
Ndoa hiyo ilikuwa ya pili kwa Pitt, hapo awali alifunga ndoa na nyota wa ‘Friends Jennifer Aniston.
Jolie, ilikuwa ni ndoa yake ya tatu, baada ya kuolewa na waigizaji Billy Bob Thornton na Jonny Lee Miller.
BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED