CEO wa Samsung, Han Jong-Hee afariki dunia

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:32 PM Mar 25 2025
Han Jong-Hee.
Picha: Mtandao
Han Jong-Hee.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya teknolojia ya Korea Kusini, Samsung Electronics, Han Jong-Hee, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63.

Kulingana na msemaji wa kampuni hiyo aliyezungumza na kituo cha habari cha CNN, Han amefariki dunia baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo (cardiac arrest) uliomsababishia umauti leo Jumanne Machi 25, 2025.

Han Jong-Hee alizaliwa mwaka 1962 na alijiunga na kampuni ya Samsung Electronics mwaka 1988 baada ya kumaliza Shahada yake ya Kwanza ya Uhandisi wa Umeme katika Chuo Kikuu cha Inha nchini Korea Kusini.

Tangu mwaka 2022, aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, akisimamia maeneo ya vifaa vya kielektroniki vya nyumbani na simu za mkononi.