NECTA yatoa ratiba ya mitihani ya ualimu Mei 2025

By Restuta James , Nipashe
Published at 06:33 PM Mar 25 2025
NECTA yatoa ratiba ya mitihani ya ualimu Mei 2025.
Picha: Mtandao
NECTA yatoa ratiba ya mitihani ya ualimu Mei 2025.

Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) limetoa ratiba ya mitihani ya ualimu, inayotarajiwa kufanyika kuanzia Mei 5, 2025, hadi Mei 14, 2025.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mtihani wa kwanza utafanyika Mei 5, ukihusisha masomo ya msingi ya ualimu, na utaendelea kwa siku kadhaa hadi kufikia Mei 14, 2025, ambapo mitihani itahitimishwa kwa masomo ya Elimu kwa Michezo na Vielelezo vya Teknolojia.

Ratiba kamili ya mitihani hiyo inapatikana kwenye tovuti rasmi ya NECTA na katika vituo vya mitihani kote nchini. Wanafunzi na walimu wanahimizwa kujiandaa ipasavyo kwa mitihani hiyo muhimu katika taaluma ya ualimu.

Ratiba.