Mbowe aonekana hadharani baada ya ukimya wa muda mrefu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:19 PM Mar 25 2025
Freeman Mbowe aonekana hadharani baada ya ukimya wa muda mrefu.
Picha: Mtandao
Freeman Mbowe aonekana hadharani baada ya ukimya wa muda mrefu.

Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ameonekana hadharani leo, Machi 25, 2025, baada ya ukimya wa muda mrefu.

Mbowe alihudhuria msiba wa Wilfred Joachim Ngure, baba mkwe wa Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, aliyeaga dunia nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Katika ibada ya kuuaga mwili wa marehemu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Boko, Mbowe ameungana na waombolezaji wengine kuifariji familia ya Mwigulu. Baada ya ibada hiyo, msafara wa mazishi umeelekea Shia, Old Moshi mkoani Kilimanjaro kwa maziko.

Kuonekana kwa Mbowe kwenye tukio hili kumewavutia wengi, kutokana na muda mrefu kuwa kimya kwenye masuala ya siasa. Hili linaibua maswali iwapo atarejea tena katika harakati za kisiasa au kupumzika.