Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, John Shibuda amekutana na kufanya mazungumzo na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuhusu masuala mbalimbali yanayogusa anachokiita "mustakabali wa taifa".
Shibuda amesema mazungumzo yake na Mbunge Mpina jijini Dar es Salaam leo ylijikita kujenga anachokiita "makutano ya fikra za agano la kale na agano jipya la kisiasa" kwa lengo la kutafakari nchi ilikotoka, ilipofika na iendako.
Alimtaka Mpina kutokata tamaa kwa kuwa hata manabii na mitume walipata changamoto za kupakwa matope kwa uongo bandia na kupumbaza uono wa macho na akili timamu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED