DC Makilagi atoa eneo kupandwa miti 2,000 ya The Guardian Ltd

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 03:02 PM May 22 2025
DC Makilagi atoa eneo kupandwa miti 2,000 ya The Guardian Ltd
Picha: Vitus Audax
DC Makilagi atoa eneo kupandwa miti 2,000 ya The Guardian Ltd

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi ametoa eneo katika shule mpya ya msingi Shadi iliyopo katika Kata ya Luchelele jijini Mwanza kwaajili ya kupandwa na kusimimiwa miti iliyotolewa na Kampuni ya The Guardian ltd.

Kati ya Miti hiyo 2,000 miti tayari kampuni imetoa miti 200 ambayo imepandwa shuleni hapo huku miti muda mfupi mara baada ya kupandwa miti 200 iliyotolewa na serikali kupitia ahadi ya Tuzo ya Mwandishi Mahiri wa habari za Mazingira iliyopandwa katika shule ya msingi Luchelele.

Akizungumza wakati wa kutoa eneo Mkuu huyo wa Wilaya ameipongeza kampuni hiyo kwa kuonesha njia ya kuongeza katika kile kilichotolewa na serikali ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kulinda na kuhifadhi Mazingira.

Kadhali ameomba kampuni hiyo kupitia wawakilishi wake waliopo jijini humo akiwemo mshindi wa Tuzo hiyo Vitus Audax kuwa sehemu ya kutembelea eneo hilo ili kuhakikisha miti inatunzwa na kufikia malengo.

Akizungumza mara baada ya kupanda miti hiyo Vitus Audax amesema Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ametoa miti kama sehemu ya kurejesha kwa jamii katika kile kilichofanywa na serikali kupitia mshindi wa Tuzo ya Samia Kalamu Awards.

“Tayari miti 200 ikiwemo ya matunda aina ya parachichi, mipera pamoja na miti ya kivuli na mbao tumeikabidhi na kuipanda katika eneo hili huku mingine ikitolewa serikali ambayo tumeipanda katika shule ya msingi Luchele,” amesema

Aidha amesema miti 1,800 itatolewa hivi karibuni na kampuni hiyo na kukabidhiwa kwa ofisa misitu wa Jiji hilo lengo likiwa ni kuendeleza kampeni ya kufikia mizi milioni 1.5 jijini humo.