Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax amesema kuimarika kwa diplomasia ya ulinzi na mataifa mengine kumesaidia nchi katika mambo mengi, ikiwamo tukio la hivi karibuni la nchi ya Kenya kuipongeza Tanzania kwa kuzuia raia wake waliotaka kuingia nchini kinyume na taratibu.
Dk.Tax amesema hayo leo Mei 22, jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka minne ya wizara yake chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema, moja ya mafaniko ambayo taifa limeyapata katika kipindi hicho cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia ni pamoja na kuimarika kwa diplomasia ya ulinzi na mataifa mengine.
“Kuimarika huku kwa diplomasia ya ulinzi ndiko kumesaidia hata tukio la hivi karibuni la Tanzania kuzuia baadhi ya watu waliotaka kujipenyeza ndani ya nchi yetu, mtu mwingine angeona labda nchi yao ingewatetea lakini tumeshuhudia wote kuwa nchi yao ndiyo imekuwa ya kwanza kuipongeza serikali yetu,” amesema Dk.Tax
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED