Chama cha Mapinduzi Wilaya Ilala imetekelezwa Ilani ya Chama hicho kwa zaidi ya asilimia 100 kwa kukamilisha na kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa mwaka 2020/2025.
Makusanyo ya mapato kwa mwaka Halmashauri Ilala yameimarika kwa sasa wanakusanya Sh. bilion.120 ambapo awali walikuwa wakikusanya Sh. bilioni 81.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho kwa kipindi cha miezi sita.
Mpogolo amesema miradi mingi imeweza kutekelezwa na kukamilika ikiwemo ya elimu, afya, miundombinu na huduma za kijamii. Ilala imeweza kutekeleza ujenzi wa maghorofa nane ya Shule za Sekondari yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 12.6 katika Kata ikiwemo ile ya Mnazi Mmoja, Minazi Mirefu, Ukonga na Kipunguni.
Akizungumzia Sekta ya Afya mkuu huyo wa wilaya amesema Serikali imejipanga kujenga vituo vya afya kila kata huku akitolea mfano wa ujenzi wa Zahanati ya kisasa ya Mzinga pamoja na ununuzi wa vifaa tiba na madawa.
Amesema Ilala imeweza kukuza na kuimarisha uchumi kwa wananchi wake kwa kutenga kiasi cha Shilingi Bilioni 18 zitakazoanza kutolewa hivi karibuni katika mikopo isiyo na riba ya asilimia kumi.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar Salaam Elihuruma Mabelya amesema wameweza kukamilisha miradi hiyo kwa kuzingatia na kupokea maelekezo kutoka ndani ya CCM kutaka kukamilika kwa miradi hiyo.
"Tuliweza kuvunja miradi yote inayosuasua kukabidhi kwa wakandarasi wengine na silaha ilikuwa ni kujuoanga kwa watendaji na viongozi wote kila mmoja asimame kutekeleza majukumu yake' amesema
Amesema Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilayani humo inatembea kifua mbele kwa kukamilisha na kutekeleza ilani kwa asilimia zote kuelekea Oktoba 2025.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED