Mchengerwa atengua uamuzi vishikwambi vya madiwani

By Cynthia Mwilolezi , Nipashe
Published at 05:56 PM Jun 20 2025
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa
Pich
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewangiza Katibu mkuu wa wizara hiyo Adlofu Ndunguru kuwandikia wakurugenzi wa halmashauri kutokuchukua vishikwambi walivyokuwa wanatumia madiwani waliomaliza muda wao pamoja na stajihiki zao.

Aidha Mchengerwa ametumia fursa hiyo kuwapongeza wakuu wa mikoa yote 26 kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya katika kusimamia miradi ya maendeo ya ambayo ni Ilani ya Chama Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Mchengerwa aliyasema hayo leo wakati akizungumza  na madiwani wa Jiji la Arusha kupitia simu ya kiganjani ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda katika kikao hicho kutokana na vishikwambi hivyo kuwa na taarifa binafsi za madiwani hao. 

"Ninatambua kwamba Machi 20 mwaka huu  ndiyo siku ya kuhitimisha utumishi katika ngazi ya madiwani katika awamu hii ya kwanza ya serikali ya awamu ya sita hivyo maelekezo yangu kwa katibu mkuu vifaa ambavyo walikuwa wanatumia madiwani vikiwemo vishikwambi waendelee kubaki navyo kwa sababu humo ndani wameweka siri zao, wameweka barua pepe zao,wameweka mawasiliano yao na ndugu zao,"amesema

Kwa mujibu wa Mchengerwa,  mafanikio yote  yanayoandika sasa na  serikali ya awamu ya sita hasa katika utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na serikali za mitaa, ni mafanikio ya pamoja kati  ya serikali kuu na serikali za mitaa ambayo yamesimamiwa  kikamilifu na na madiwani kote nchini.

"Msingi wa kazi kubwa ya nguvu na jasho, ufundi na ustadi iliyofanywa na madiwani kote nchini wakizisimamia halmashauri kote nchini imeandikwa katika kitabu cha dhahabu kwa sababu wametumikia nchi hii kwa uzalendo kwa  watanzania wanyonge, wakawaida, wanaanchi wa vijijini, mijini. 

Aidha Makonda  ametumia fursa kuwasisitiza wakurugenzi wa halamshauri zote za mkoa wa Arusha kuwalipa madiwani stahiki zao zote yakiwemo mafao yao kwa wakati kwa sababu ni takwa la kisheria  na kama kuna cjangamoto yeyote wawasiliane na ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha.

Kuhusu posho za  wenyeviti wa Mitaa, Vijiji  na Vitongoji ziingizwe kwenye akaunti zao za benki moja kwa moja tofauti na hivi sasa ambapo zinatumwa ofisi za watendaji wa Kata ikiwa ni pamoja na kupeleka nakala  miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao yote katika bajeti ya kila mwaka wa fedha kuanzia mwaka huu wa 2025-2026 ili waifahamu vizuri na kila mtendaji wa serikali akitaka kutekeleza mradi katika maeneo yao  lazima viongozi hao wapate taarifa.

Kuhusu madiwani wa Mkoa wa Arusha wanaomaliza muda wao alisema  ushirikiano wao  umewezesha miradi kutekelezeka na kukipa ujasiri Chama cha Mapinduzi (CCM) katika miradi mbalimbali inayotelezeka kwani kila maeneo ya Jiji hilo wakandarasi wapo kazini kutokana na ujenzi wa miradi ikiwemo ongezeko la mapato

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude  amewataka madiwani hao wanaomaliza muda wao kuendelea kusemea kazi za serikali zilizofanywa na Rais Samia Hassan Suluhu katika kila kata za Jiji hilo. 

Amesisitiza miradi isiyokamilika serikali itasimamia ikiwemo kivuko kiaichojengwa ilhali fedha zipo kwenye akaunti kata ya Ferrari, Osunyai korongo inasemekana mkandarasi kaondoka bila kujenga hivyo yeye  hatakuwa mpole, atahakikisha kazi site zilizopaswa kumalizwa zitasimamiwa

 Mkurugenziwa Jiji la Arusha, John Kayombo amewataka madiwani wa Jiji la Arusha kutoka kata zote  25 waliomaliza muda wao wa udiwani kutumia baraza hili kuaga na si kuomba miradi 

"Ageni msiombe miradi, tumieni baraza hili kuagana na kushukuru kwa kukaa katika baraza hili kwa miaka mitano tunatamani mrudi kama mlivyo basi tuwatakie kila la heri,"amesema

Wakati huo huo,  Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe ametoa nafasi kwa baadhi ya madiwani kutoa shukrani zao ambapo Diwani wa Kata ya Themi, Lobora alishukuri Jiji la Arusha kwa kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya kata zao  ikiwemo kuomba msamaha kwa baadhi ya watendaji lengo ni kuhakikisha maendeleo yanapatikana.