TAKWIMU ya idadi ya waumini wa kanisa katoliki katika kipindi cha mwaka 2025 imeongezeka kutoka bilioni 1.39 mwaka 2024, hadi kufikia bilioni 1.406 katika kipindi cha mwaka 2025.
Katika kipindi hicho, Baba Mtakatifu ameunda majimbo makuu matatu; ameunda majimbo mapya saba, likiwamo Jimbo Katoliki la Bagamoyo “Dioecesis Bagamoyensis” pamoja na kuunda Jimbo jipya la Kitume.
Kuunda majimbo hayo ni kusogeza huduma za kichungaji Karibu na watu wa Mungu mahali walipo.
Kwa mujibu chombo cha habari Vatican, Roma, taarifa imesema dadi ya mapadre barani Afrika, imeongezeka kwa asilimia 2.7 na maaskofu wameongezeka pia barani humo.
Nchi zinazoongoza kwa idadi kubwa ya waamini wa Kanisa Katoliki barani Afrika ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ikiwa ni wakatoliki milioni 55.
Inafuata Nigeria waamini milioni 35 na kuna nchi ambazo pia zina idadi kubwa ya waamini wa Kanisa Katoliki ni kutoka Afrika Mashariki, Uganda, Tanzania na Kenya.
Kadhalika, ukuaji wa waamini wa Kanisa Katoliki Barani Afrika ni sawa na asilimia 3.31
Pia, idadi ya maaskofu wenye dhamana ya kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu imeongezeka kwa asilimia 1.4 kutoka maaskofu 5,353 hadi kufikia 5,430.
Idadi ya maaskofu barani Afrika imeongezeka kutoka asilimia 13.8 hadi asilimia 14.2 ya mwaka 2023.
Kanisa Katoliki lina majimbo makuu 3, 041 na majimbo 406, 996. Idadi ya Mapadre Barani Afrika imeongoza kwa asilimia 2.7.
Idadi ya Mashemasi wa kudumu katika kipindi cha Mwaka 2023 imeongezeka kutoka Mashemasi 50,150 hadi kufikia Mashemasi 51, 433.
Takwimu zinaonesha kwamba, kuna idadi ndogo sana ya mashemasi wa kudumu barani Afrika.
Idadi ya watawa wa kiume na wa kike inaendelea kupungua, ingawa idadi hii barani Afrika inaendelea kuongezeka, lakini athari kubwa inajionesha barani Ulaya.
Idadi ya watawa imepungua kutoka watawa katia kipindi cha mwaka 2023, na barani Afrika kuna ongezeko la asilimia 2.2.
Idadi ya waseminari walioko Seminari kuu imepungua kwa asilimia 1.8 yaani kutoka kwa Waseminari 108,481 hadi kufikia idadi ya waseminari 106,495, lakini Barani Afrika idadi ya waseminari imeongezeka kwa asilimia 1.1 kutoka waseminari 34,541 hadi kufikia waseminari 34,924.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED