Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameagiza wachimbaji wadogo na wa kati wa madini nchini kutumia masoko ya ndani na vituo vilivyowekwa na serikali kuuza madini yao badala ya kufanya utoroshaji kwenda nje ya nchi ili kusaidia kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia sekta hiyo.
Majaliwa, amesema hayo leo Juni 24, 2025 jijini Dodoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mitambo ya wachimbaji wadogo na vitendea kazi vya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
“Wachimaji wadogo na wa kati endeleeni kuuza madini katika viwanda vyetu vya kusafisha dhahabu ili kuendelea kuchochea ukuaji wa uchumi nchini na wale ambao wanahusika na usafirishaji wa madini nendeni mkauze kwenye masoko yetu 43 tuliyaweka na vile vituo 109.
“Ili tujiridhishe madini mzunguko wake ndani ya nchi unaanza kunufaisha taifa letu badala ya kutorosha madini unapeleka nje ya nchi manake nini unakwenda kunufaisha nchi hiyo,”amesema Majaliwa
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED