Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani imepokea msaada wa samani za ofisi kutoka kwa mdau wa maendeleo, Dk. Charles Mwamaja kutoka Wizara ya Fedha.
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya mdau huyo, Philemon Maliga amesema samani hizo ni ishara ya ushirikiano kati ya waandishi wa habari na wadau wa maendeleo kwa lengo la kuboresha mazingira ya kazi ya waandishi.
Maliga amesema waandishi wa habari ni chombo muhimu kwa jamii kwa kuwa hutoa elimu na taarifa, hivyo wanapaswa kuungwa mkono katika kutatua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Harold Shemsanga amemshukuru mdau huyo kwa msaada huo ambao amesema umesaidia kupunguza changamoto za ofisi na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo kwa kuwasaidia waandishi wa habari kuboresha mazingira yao ya kazi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED