Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ameifungua milango ya fursa za kiuchumi jijini Dodoma kwa kuhakikisha uwanja wa ndege Msalato unakamilika pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa ya (SGR).
Makalla ameyasema hayo leo Juni 24,2025, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Dodoma mjini, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake.
Amewaeleza wananchi kuwa uwanja wa ndege wa Msalato unakwenda kukamilika na tayari ndege ya majaribio imeshatua uwanjani hapo.
Amesema wakandarasi wa kujenga reli kisasa Dodoma- Makutupora- Tabora- Isaka hadi Mwanza wanaendelea na kazi ya kuhakikisha wanaikamilisha.
Makalla amewaahidi wananchi kuwa milango mingi ya fursa za kiuchumi itaendelea kuwapo kupitia miradi inayotekelezwa.
“Miradi mbalimbali aliyosema Mkuu wa Mkoa hapa ni matokeo ya uongozi mzuri wa Rais Samia Suluhu Hassan. Itoshe kusema tunakushukuru wananchi kwa kuunga mkono Chama Cha Mapinduzi,” amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED