Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema jumla ya majimbo ya 272 ya yatatumika katika uchaguzi wa Wabunge kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambengele, amesema hayo leo Mei 12, jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya ugawaji wa majimbo hayo mapya ya uchaguzi na ubadilishaji wa majina.
“Kutokana na ongezeka kwa majimbo mapya nane katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, jumla ya majimbo 272 yatatumika katika uchaguzi wa wabunge katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya majimbo hayo 222 yapo Tanzania bara na 50 Zanzibar orodha ya majimbo yote itachapishwa na kutangwa kwenye gazeti la serikali,amesema
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED