Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, CPA Amos Makalla, amewahakikishia wananchi wilayani Muleba, mkoani Kagera, kuwa serikali itaendelea kutekeleza miradi ya kuwaletea maendeleo, na waishio katika kisiwa uboreshaji vyombo vya usafiri utaendelea ili wawe salama.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani humo wakati akiendelea na ziara yake ya siku saba.
Katika mkutano huo, Makalla amewahakikishia usalama wananchi wanaoishi katika visiwa kuwa serikali itaendelea kuboresha vyombo vya usafiri ili wawe salama.
“Tunaahidi tutaendelea kushirikiana nanyi katika kutatua changamoto na kuwaletea maendeleo. Imani mliyonayo kwa CCM inatokana na wajibu uliopewa chama kwa wananchi,” amesema.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameweka alama Muleba ambapo iko miradi inayotekelezwa ya afya na maji.
Amesema mradi wa maji wa kimkakati wa Sh. bilioni 39 unakwenda kuchukuliwa Ziwa Victoria na kutekelezwa wilayani humo ambapo kila maeneo miradi itapita.
Amewataka wananchi wanaowakejeri hasa mwanasiasa wakati wa kuelekea kipindi cha uchaguzi ni kuachana nao na kukichagua CCM.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED