Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, CPA Amos Makalla, ametoa kauli kuhusu kelele za mitandaoni kuzuiwa mwanaharakati Martha Karua wa Kenya na wenzake kuingia nchi, akisema hawawezi kulazimishwa kwa kuwa Tanzania ni nchi huru, yenye dola kamili na mamlaka kamili, haiwezi kuruhusu hilo kwa shinikizo.
Amesisitiza kuwa hakuna sheria yoyote duniani inayoweza kulishinikiza taifa huru, likiwamo Tanzania kwamba washinikize mtu fulani apokelewe.
Akizungumza leo na wananchi wa Mji wa Katoro, mkoani Geita, katika mkutano wa hadhara wakati akiendelea na ziara yake ya siku saba.
Makalla amesema watu wote wenye hila na milango ya uchochezi ya kuwagawa Watanzania hawana nafasi katika taifa la Tanzania.
“Hata hili nafikiri nilisemee hapa, kwenye mitandao ya kijamii tunaona heeh sijui mwanaharakati Martha Karua wamezuiwa uwanja wa ndege walikuwa wanakuja kwenye kesi ya Tundu Lissu.“Nataka niseme, Tanzania hii ni nchi huru, ni dola iliyokamilika, yenye mamlaka kamili, inayouwezo wa kuruhusu au kutoruhusu mgeni yeyote kuingia Tanzania,” amesema.
Makalla amesema hawawezi kulazimishwa kwa kuwa Tanzania ni nchi huru, yenye dola kamili na yenye mamlaka kamili, haiwezi kuruhusu hilo kwa shinikizo kwamba, ‘tunaomba huyu aruhusiwe kuingia Tanzania’,” amesisitiza.
Makalla amesema hakuna sheria yoyote duniani inayoweza kulishinikiza taifa huru, likiwamo Tanzania kwamba, washinikize mtu fulani apokewe.
Kadhalika, amesema Idara ya Uhamiaji inayo mamlaka ya kuruhusu au kutoruhusu mtu wa kigeni kuingia nchini kwa sababu wanazingatia sheria na kanuni.
"Tumemshtukia, tumeshtuka yeye ni mwanaharaki wana rekodi Kenya hazijafutwa, Tanzania ni nchi salama na ya mfano, uhusiano wetu na Kenya ni wa kihistoria tutaendelea kushirikiana na Wakenya na si kwa sababu ya Martha Karua, mahusiano ni mazuri kuliko wakati wowote na sisi ni ndugu," amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED