Makalla: Mradi wa EACLC kukuza uchumi Tanzania

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 06:06 PM Jul 15 2024
Kituo cha biashara na Usafirishaji  Afrika Mashariki (EACLC).
Picha: Romana Mallya
Kituo cha biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC).

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa Amos Makalla, amesema mradi wa Kituo cha biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo mkoani Dar es Salaam kuchochea ukuaji wa uchumi.

Makalla amesema hayo leo baada ya kutembelea kituo hicho leo kujionea mradi huo unaoendelea kujengwa.

Amesema kituo hicho kinakwenda kuwa kiunganishi kati ya China na Afrika Mashariki, kwa kuwa  kutakuwa hakuna haja ya kwenda China.
Makalla amesema bidhaa zitapatikana Tanzania na kuchochea ukuaji wa maendeleo.

"Kituo hiki kitakwenda kukuza uchumi ndani ya Afrika Mashariki hasa Tanzania,  hivyo tumpongeze Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuukwamua mradi huu mkubwa sana ambao utaongeza ajira, kwani maduka 2060 yapo hapa. Kila Mtanzania ana fursa ya kuwekeza hivyo vyovyote vile wenyeji tutafaidi zaidi," anasema.

1

Makalla ametembelea pia, mradi wa jengo la wazazi la Hospital ya Sinza Palestina ambalo lipo mbioni kumaliza.

Amesema Hospitali hiyo ya  imekua na wameshuhudia maboresho makubwa yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

"Tunaojua Sinza Palestina ilianza kama zahanati na sasa kuna mabadiliko. Leo wanalaza wagonjwa, watoto wadogo wanaozaliwa pasipo utimilifu hakuna rufani wanatibiwa hapa huduma nyingi na vifaa vya kisasa vipo hapa Sinza Wilaya ya Ubungo tunakila sababu ya kuipongeza serikali yetu kwa utekelezaji wa Ilani," amesema.