Nchini Canada, sheria imeruhusu mtu kusaidiwa kufa tangu mwaka wa 2016, nchi hiyo kwanza ilipoanzisha sheria inayoruhusu maombi ya kusaidiwa kufa kwa watu wazima walio na magonjwa yasiyotibika ambayo husababisha mateso yasiyovumilika au wagonjwa mahututi.
Mnamo mwaka 2021, kanuni zililegezwa ili kuruhusu wagonjwa wasio na magonjwa yasiotibika ambao wanaugua sana pia kusaidiwa kufa.Na kuna mipango ya kuwezesha kusaidia kufa watu wazima walio na magonjwa ya akili pekee, bila hali zingine, ndani ya miaka miwili.
Daktari Stefanie Green, mtaalam wa suala hili na aliyejitolea kwa miaka kusaidia wagonjwa wanaotaka kufa, anaakisi jambo ambalo linaweza kuonekana kama kinzani kwa wengi: wazo la daktari kusaidia wagonjwa kufa.
"Watu wengi wanafikiri jukumu letu kama madaktari ni kuokoa maisha, na kwa kiasi fulani hiyo ni kweli. Lakini nadhani kiini cha kile ambacho daktari hufanya ni kuwasaidia watu, tunasaidia watu kupambana na magonjwa, lakini mara nyingi hatuna chochote cha kuwasaidia nacho. Tunakumbana na magonjwa ambayo hatuwezi kukabiliana nayo na kufanikiwa. Na jukumu letu si kuwatelekeza wagonjwa, ninaamini jukumu la daktari ni kusaidia watu katika hatua zote za maisha yao, na kusaidiwa kufa ni sehemu ya hilo." anasema Daktari Stefanie Green
Stefanie Green ana umri wa miaka 56. Alianza maisha yake ya kitaaluma akifanya kazi kama daktari mkuu na baadaye akajitolea kutunza wanawake wajawazito, kuwasaidia wakati wanajifungua, na watoto wachanga wanapozaliwa.
Baada ya zaidi ya miongo miwili katika tasnia hiyo, mnamo mwaka 2016, wakati sheria ya Canada ilipoanza kuruhusu raia kusaidiwa kufa, Green alibadilisha mwelekeo wake wa kazi. Leo anatumia 75% ya wakati wake kusaidia watu kufa.Namna nilivyobadili mtazamo
Green anaeleza kwamba anaona kuna ufanano mkubwa kati ya ujuzi unaohitajika kwa madaktari na kusaidia mgonjwa kufa. Kwake yeye, wakati wa kuzaliwa na kifo cha mtu, jukumu la daktari ni kuwa mwongozo katika mchakato wa asili.
Lakini alipoulizwa kwa nini alibadili mtazamo wake hadi kusaidia watu kufa, alitaja mambo kadhaa. "Nilipinga sana wazo la kuacha kazi niliyokuwa nikifanya wakati nasaidia wanawake kujifungua," anasema. "Sikuweza kufikiria kitu kingine chochote ambacho kinaweza kunifurahisha kama hicho."
Hata hivyo, anasema kadiri miaka ilivyosonga, ilizidi kuwa vigumu kwake kijihisi sawa kutokana na zamu ndefu anapokuwa kazini akisaidia kina mama kujifungua. Ilikuwa katika kipindi hiki ambapo Canada ilihalalisha kusaidia watu kufa. Green anasema alikuwa amefuatilia majadiliano kwa karibu mno.
"Kwa miaka 25 ya uzoefu wa kliniki, nimeona vifo vingi. Vifo vizuri, lakini pia vifo vibaya," anasema. Siku chache baada ya sheria kuanza kutekelezwa, mgonjwa wa kwanza aligonga mlango wake. "Niko tayari, alisema."
"Bila shaka ilikuwa wakati wa kipekee. Ilikuwa kitu kisicho cha kawaida na hakika sitasahau wakati huo," anasema."Nina bahati sana na ninashukuru kufanya kazi na mgonjwa huyo na familia yake akiwa wa kwanza."
Anasema alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kusaidia watu kufa nchini Canada. Harvey alikuwa mtu wa kipekee, anakumbuka. Alikuwa mgonjwa sana na kuna uwezekano mkubwa angekufa ndani ya wiki chache.
"Alikuwa mtu mwenye fikra za asili kabisa. Alikuwa akingojea tu mabadiliko ya sheria na yalipofanyika, akaja mlangoni kwangu akiwa na karatasi mkononi huku akisema, 'Hiki ndicho ninachotaka'."
Alikuwa anaungwa mkono na jamaa zake. Harvey alilala kwa mara ya mwisho akitazama machoni mwa mkewe, ambaye alikuwa ameuoa kwa miaka 52.
Vifo, kama kuzaliwa, ni hali za kipekee, anasema daktari. "Kwa sababu watu ni wa kipekee." Lakini baada ya miaka mingi ya kufanya kazi hii, anasema kuna utaratibu ambao huwa anaufuata kwa wagonjwa wote.
Kabla ya kuelezea mchakato huo, Green anaelezea njia mbili zinazotumiwa nchini Canada kumsaidia mgonjwa kufa. Njia ya kwanza ambayo ni nadra sana kutumika, daktari humpa mgonjwa dawa ya barbiturate yenye nguvu. Mgonjwa mwenyewe hunywa kioevu hicho na kulala usingizi, kisha hupoteza fahamu na kufa ndani ya nusu saa.
"Ile inayotumika na wengi, anaelezea, ni dawa ambayo daktari humdunga mgonjwa kwenye mshipa." Dawa nne hutumiwa. Ya kwanza, ni dawa ya wasiwasi, hutumiwa kumfanya mgonjwa atulize akili yake.
"Ni kipimo cha juu na asilimia 98 au 99 ya wagonjwa hulala. Dalili zao hupotea, na kuhisi vizuri." Dawa ya pili, ni ya hiari, ni kutia ganzi mshipa ambapo dawa itawekwa. Green anasema ni njia ambayo huwa anaitumia.
Dawa ya tatu inatumika kumlaza mtu wakati wa upasuaji. Ikiwekwa kwa kiwango cha juu, humfanya mgonjwa kupata usingizi mzito, kisha anapoteza fahamu kabisa. Wakati hii inatokea, kupumua kwa kawaida hupungua na kuacha. Watu wengi hufa baada ya dawa ya tatu, lakini Green anasema madaktari hawategemei hio.
"Wana data nyingi za usalama, kwa hivyo, tunatumia dawa ya nne ambayo inasumbua harakati za misuli kwenye mwili."Kwa hiyo, natumia dawa hizi nne na ninajua zikidungwa kwenye mshipa wa mgonjwa atakufa," anasema.
"Hii ni njia ya kikatili ya kuielezea, lakini ndivyo inavyotokea."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED