Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, Amos Makalla,amekijibu CHADEMA kwamba, isiseme uongo kwamba utawala umepinga No Reforms No Election, hilo limepingwa na wana CHADEMA wenyewe wakianza na G55, vyama 17 wanaojitambua watakaoshiriki uchaguzi.
Kadhalika, amewaeleza kuwa uimara wa chama haupimwi kwa uongozi, bali idadi ya wanachama.
Makalla akizungumza leo Mei 23,2025, Shinyanga Mjini katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya kikazi kwa mikoa saba, alisema amefuatia Kamati Kuu CHADEMA imekutana.
“Makamu Mwenyekiti CHADEMA, John Heche, ametupa takwimu kwamba CHADEMA haina mgogoro wako imara, lakini katika Kamati Kuu ameainisha idadi ya waliohama akiwamo mjumbe wa Kamati Kuu na wanachama wao.
“Kwa hiyo jumla waliohama CHADEMA ni 55, alafu Heche amehitimisha kwa kusema CHADEMA iko imara.Nataka nimfundishe Heche uimara wa chama haupimwi kwa uongozi, uimara wa chama au ukubwa wa chama unapimwa kwa idadi kubwa ya wanachama, asiongopee watu, wana CHADEMA kimekimbiwa na maelfu ya wanachama na kinasambaratika, hawa kifo tayari,” amesema.
Makalla amesema amesikia kauli ya pili kutoka kwa Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika, akisema kaulimbiu yao No Reforms No Election imepingwa vikali na utawala.
“Ninamwambia acha uongo, imepingwa na CHADEMA wenyewe wakianza na G55 wamepinga, kundi la pili ni la vyama 17 wanaojitambua wanashiriki uchaguzi
Kundi la tatu ni la wananchi wanajitambua wanajua uchaguzi ni kwa mujibu wa katiba, asisingizie dola,” amesema
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED