Miaka minne ya Samia mifugo yafikia milioni 190

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:43 AM Jul 05 2025
Mifugo
PICHA: MTANDAO
Mifugo

Tangu aingie madarakani mwaka 2021, Rais Samia Suluhu amechukua hatua za makusudi kuinua sekta ya mifugo ili kuleta tija na kuinua maisha ya wafugaji , hatua alizozichukua ni pamoja na kuongeza bajeti ya sekta hii kutoka Sh.bilioni 168 mwaka 2021/2022 hadi Sh bilioni 460 mwaka 2024/2025.

Serikali pia imeboresha ubora wa uzalishaji wa mbegu za malisho jitihada hizi zimesaidia uzalishaji wa mbegu za malisho ambao umeongezeka kutoka tani 127.8 mwaka 2023/2024 hadi tani 152.67 mwaka 2024/2025. Idadi ya mifugo pia imeongezeka hadi milioni 190.

Ongezeko hilo limechangia kuongeza uzalishaji wa nyama kutoka tani 963,856 mwaka 2023/2024 hadi tani 1,054,114 Februari mwaka huu ma pia thamani ya nyama iliyozalishwa imeongezeka kutoka Sh trilioni 7.71 mwaka 2023/24 hadi Sh trilioni 8.43 mwaka 2024/25.