Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete ametembeela banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam na kujionea jinsi wanachama na wananchi wanavyohudumiwa.
Kikwete ambaye aliambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Patrobas Katambi, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhra Yunus, alielezwa jinsi wanachama na wananchi wanavyohudumiwa katika banda hilo.
Amefurahishwa na taarifa ya namna wanachama wanavyofurahia huduma za PSSSF Kidijitali ambazo zimepelekea mapinduzi makubwa katika utoaji wa huduma.
Pia Mhe. Kikwete alijionea bidhaa bora za viatu, mikoba na mikanda vinavyozalishwa kwenye kiwandha cha KLICL ambacho PSSSF imewekaza.
Halikadhalika alijionea nyama safi inayotoka kwenye Machinjio ya Kimataifa ya Nguru Hills Ranch, ambayo PSSSFni muwekezaji mkubwa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED