Tanzania yatajwa nchi yenye amani zaidi Afrika Mashariki

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:07 PM Jul 04 2025
Tanzania yatajwa nchi yenye amani zaidi Afrika Mashariki
Picha:Mtandao
Tanzania yatajwa nchi yenye amani zaidi Afrika Mashariki

Tanzania imeendelea kung’ara kama taifa linaloongoza kwa amani katika Afrika Mashariki, kwa mujibu wa Ripoti ya Global Peace Index (GPI) ya mwaka 2025, ambapo imeshika nafasi ya 73 kati ya mataifa 163 duniani.

Pamoja na mafanikio hayo kikanda, ripoti hiyo imebainisha kuwa Tanzania imeshuka kwa nafasi nane kimataifa, ikilinganishwa na nafasi ya 65 iliyokuwa nayo mwaka 2024.

Global Peace Index ni ripoti inayotolewa kila mwaka na taasisi ya Institute for Economics and Peace (IEP), ikipima kiwango cha amani kwa kutumia vigezo mbalimbali kama vile usalama wa jamii, migogoro ya ndani na nje, pamoja na kiwango cha kijeshi.

Katika Afrika Mashariki, Tanzania imewashinda majirani zake wote, ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, na Sudan Kusini, ambao wengi wao wameendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama na kisiasa.

Hata hivyo, kushuka kwa nafasi kimataifa kunatajwa kuchangiwa na mabadiliko katika viashiria vya usalama wa ndani, matumizi ya kijeshi na mwenendo wa kisiasa kimataifa, ingawa Tanzania bado inahifadhi taswira ya taifa tulivu na lenye mshikamano.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameshauri kuimarishwa kwa misingi ya haki za binadamu, utawala wa sheria, na ushirikishwaji wa wananchi ili kuimarisha zaidi hali ya amani na demokrasia nchini.

Ripoti hiyo ya GPI hutumika na mataifa, mashirika ya kimataifa, na wawekezaji kama kiashiria cha hali ya utulivu katika nchi mbalimbali duniani.

Rais Samia Suluhu Hassan.
🔹 Viwango vya Amani Afrika Mashariki (2025):

1. 🇹🇿 Tanzania (73)
2. 🇷🇼 Rwanda (91)
3. 🇺🇬 Uganda (113)
4. 🇰🇪 Kenya (127)
5. 🇧🇮 Burundi (133)
6. 🇨🇩 DRC (160)
7. 🇸🇸 Sudan Kusini (161)

tz.png 303.96 KB