Stand United waambulia kichapo bao 3-1 dhidi ya Fountain Gate

By Marco Maduhu , Nipashe
Published at 08:05 PM Jul 04 2025
Stand United waambulia kichapo bao 3-1 dhidi ya Fountain Gate
Picha: Marco Maduhu
Stand United waambulia kichapo bao 3-1 dhidi ya Fountain Gate

Mechi ya kwanza kati ya Stand United na Fountain Gate,imemaliza, huku Fountain Gate wakiibuka na ushindi wa bao 3-1

Mchezo huo wa Play Off umechezwa leo Julai 4,2025 katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga, ambapo mchezo wa marudiano utachezwa Julai 8 huko Singida, ambapo mshindi atashiriki kucheza masimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Goli la kwanza la Fountain Gate limefungwa kipindi cha kwanza na mchezaji Kasim Haroon dk 28 ,huku Stand United wakisawazisha dk ya 44 goli liliofungwa na Joram Mgeveke.

Kipindi cha pili Fountain Gate waliongeza Goli,lililofungwa na Said Sadiki dk 65.

Ambapo Goli la tatu lilifungwa na Mudrick Gonda dk 82.

Baada Goli hilo kufungwa,iliibuka vurugu na kusababisha mpira kusimama kwa muda.

Hadi dakika 90 zinamalizika Fountain Gate walibakia na Goli zao 3-1