Othman afika Kisiwa Panza kuusaka Urais 2025

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:36 PM Apr 29 2025
Othman afika Kisiwa Panza kuusaka Urais 2025
Picha:Mpigapicha Wetu
Othman afika Kisiwa Panza kuusaka Urais 2025

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Othman Masoud Othman akiambatana na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar Ismail Jussa Ladhu wamefanya ziara ya ujenzi wa Chama eneo la kisiwa Panza kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

Ziara hiyo ya kisiwani  imefanyika leo 29 April 2025 ni ya kwanza tangu kwa Othman Masoud Othman ni yakwanza tangu kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho.

Akizungumzia kuhusu ziara hiyo Katibu wa Habari na Uenezi Salim Bimani amesema kisiwa Panza ni eneo muhimu ambalo linapaswa kufanywa siasa kwa muda wote.

Amesema ujio wa Mwenyekiti wa Chama Taifa utaleta hamasa zaidi na kuamsha ari ya wananchi wa kisiwa hicho ambazo muda mrefu wamekua wafuasi wa Chama chao.

Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Mkoani Mohamed Abdalla amesema kisiwa Panza ni eneo la kihistoria kwa siasa za upinzani

Amesema Wananchi wa eneo hilo wamekua wakikabiliwa na kadhia nyingi zikiwemo za kunyimwa haki zao za msingi za kupatiwa kitambilisho vya (Zan ID).

Amesema Wananchi wanamatumaini mkubwa na Othman Masoud kuwa Rais wa Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu wamiamini kuwa changamoto zao zitatuliwa na kuishi kwenye mazingira Bora.