Tuzo ya Kijana Mwenye Ushawishi Barani Afrika yamfikia Rais Samia

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:09 PM Apr 29 2025
Tuzo ya Kijana Mwenye Ushawishi Barani Afrika yamfikia Rais Samia
Picha: Mpigapicha Wetu
Tuzo ya Kijana Mwenye Ushawishi Barani Afrika yamfikia Rais Samia

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika Picha ya pamoja na Mtanzania Steven Magombeka maarufu kama Kasampaida ambae hivi karibuni alishinda Tuzo ya Vijana Wenye Ushawishi Barani Afrika, akikabidhi Tuzo hiyo kwa Rais Ikulu ya Chamwino Dodoma leo April 29,2025.

Itakumbukwa Magombeka alishinda Tuzo hiyo Aprili  12,2025 jijini Accra Nchini Ghana na leo ameiwasilisha tuzo hiyo kwa Rais Samia kama shukrani kubwa kwa mchango wake wa kuendelea kuwainua vijana mbalimbali katika sekta mbalimbali nchini.

Aidha Magombeka amemkabidhi Rais Samia zawadi ya picha aliyompiga mnamo Februari 15,2024 wakati wa ziara Nchini Norway kama sehemu ya kumbukumbu ya picha alizowahi kumpiga Rais Samia.

Tuzo hizo mashuhuri zinawatambua vijana wajasiriamali bora, wanaharakati, waleta mabadiliko na wafuatiliaji ambao wameonyesha ubora wa kipekee katika nyanja zao Kukiwa na takriban uteuzi wa vijana 5,000 kutoka nchi 52 za ​​Afrika.

Pongezi za dhati kwa Vijana 100 Wenye Ushawishi zaidi wa 2025! Mafanikio yako bora yanaendelea kutia moyo na kuleta mabadiliko katika bara zima na kwingineko.