Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wanne wa mashirika ya Serikali.
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Aprili 29, 2025 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka imesema walioteulwa ni wenyeviti wa bodi.
Rais Samia amemteuwa Dk.Fatma Kassim Mohamed kuendelea na wadhifa wake kama Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kwa kipindi cha pili mfululizo.
Pili, Dk. Jilly Maleko ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), akichukua nafasi ya Balozi Begum Karim Taj ambaye amemaliza muda wake wa uongozi.
Pia, Rais Samia amemteua Profesa Eliakimu Zahabu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (National Carbon Monitoring Center - NCMC), taasisi inayohusika na masuala ya mabadiliko ya tabianchi.
Aidha, Lucas Mwino, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), akichukua nafasi ya Dk John Mduma aliyemaliza muda wake," taarifa hiyo inaeleza.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED