PDPC yataka vyama vya siasa kujisajili, kulinda taarifa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:31 PM Apr 29 2025
Mkurugenzi wa PDPC,Emmanuel Mkilia.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkurugenzi wa PDPC,Emmanuel Mkilia.

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), imesema ni lazima kwa vyama vya siasa kujisajili kwa kuwa wanakusanya na kuchakata taarifa binafsi za watu.

Hayo yamesemwa leo Aprili 29,2025 Jijini Arusha katika mjadala wa mamlaka za udhibiti katika sekta ya habari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa habari 2025 na Mkurugenzi wa PDPC,Emmanuel Mkilia.

"Ikiwa vyama vya siasa havitajisajiii kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi no 11 ya 2022 wasipofanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria ya taarifa bianfsi,"amesema.


Kuhusu, kujisajili kwa hiyari ambao mwisho ni kesjo Aprili 30,2025, amesema ni muhimu kila mmoja anayehusika na kuchakata taarifa za watu kutimiza matakwa ya kisheria.

"Kama hujajisajili unachakata na kukusanya taarifa za watu,mtu akilalamika umetumia taarifa umekusanya taarifa zako na tume itaendelea kupambana nawe kwa mujibu wa sheria,"amesema Mkilia.