Shule ya Benjamin Mkapa yakumbukwa mashine kukuzia maandishi
By
Mwandishi Wetu
,
Nipashe
Published at 06:07 PM Apr 29 2025
Picha: Mpigapicha Wetu
Chuo cha Elimu ya Biashara CBE walipokabidhi msaada kwa shule ya Benjamin Mkapa ya jijini Dar es Salaam. Msaada huo ni pamoja.na mashine ya kukuzia maandishi kwa wenye uoni hafifu na vifaa vya kusaidia wenye usikivu hafifu.
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 4.4 kwa shule ya elimu jumuishi ya Benjamin Mkapa ya jijini Dar es Salaam.
Chuo cha Elimu ya Biashara CBE walipokabidhi msaada kwa shule ya Benjamin Mkapa ya jijini Dar es Salaam. Msaada huo ni pamoja.na mashine ya kukuzia maandishi kwa wenye uoni hafifu na vifaa vya kusaidia wenye usikivu hafifu.Miongoni mwa msaada huo ni mashine ya kukuzia maandishi kwa wanafunzi wenye uoni hafifu, vifaa vya kusaidia usikivu kwa wenye usikivu hafifu (hearing aid) na wanafunzi wenye ualbino.
Msaada huo umekabidhiwa leo na Mkuu wa chuo hicho Profesa Edda Tandi Lwoga kwa Mkuu wa shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa, Joseph Deo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Profesa Lwoga ameomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia shule hiyo kwani inamahitaji mengi.
Amesema chuo hicho nkikongwe nchini ni mashuhuri kwa kutengeneza wataalamu wa kozi mbalimbali za masuala ya biashara pamoja na teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na metrolojia.
Amesema CBE imezungukwa na shule nyingi za sekondari na kwamba kila mwaka wamekuwa wakianisha shule ambazo huenda kutoa msaada kama sehemu ya kurudisha faida kwa jamii inayowazunguka.
“Tunaona umuhimu wa kuboresha mazingira ya kusomea kuanzia huku chini kwenye sekondari kwasababu tunaamini elimu ikiboreshwa kuanzia huku chini huku juu mambo yanakuwa rahisi tu,” amesema
“Mwaka huu wakati tunasherehekea siku ya jinsia tuliainisha mahitaji ya shule ya Benjamin Mkapa na tuliona mlivyo na mahitaji mengi sana tukaona hii ni shule muafaka ya kupata msaada wa CBE kwasababu inawanafunzi wengi mahitaji maalum,” amesema Prof Lwoga
Mkuu wa shule hiyo, Joseph Deo ameishukuru CBE kwa msaada wa mashine ya kukuza maandishi kwani walikuwa wanajipanga kutafuta fedha za kununua mashine hiyo.
Amesema kwa muda mrefu wanafunzi wenye uoni hafifu walikuwa wanapata shida kwa hiyo mashine hiyo ni ukombozi kwao kwani wataweza kusoma kama wenzao wasio na matatizo ya uoni.
“Sisi tulileta maombi ya vitu vingi sasa tukadhani mtachagua kusaidia vitu vidogo vidogo lakini mmechagua kutusaidia kitu kikubwa san asana mashine ya kukuzia maandishi ndiyo ilikuwa inatuumiza kichwa tunaipataje tunawashukuru sana,” amesema
Amesema shule hiyo ina wanafunzi 160 wenye usikivu hafifu hivyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kusaidia shule hiyo ili wanafunzi wenye uoni na usikivu hafifu wapate vifaa vya kuwasiaidia kwenye masomo.
“Kwa msaada huu wa mashine ya kukuzia maandishi hawa wanafunzi watafanya vizuri darasani kwasababu watakuwa wanafuatilia masomo kama wenzao na wale wenye usikivu hafifu vifaa vilivyotolewa vitawasaidia, tunaomba wadau wengine nao wajitoleee maana wanafunzi 120 bado wanahitaji vifaa vya aina hiyo,” amesema.
Mkuu wa Kitengo cha Wanafunzi Wenye Majitaji Maalum shuleni hapo, Alfonsi Tangaza, amesema kuna shule nyingi zenye mahitaji maalum lakini hatua ya CBE kuona shule hiyo kama kipaumbele chao ni jambo ambalo limewafariji sana.