Jeshi la Polisi Nchini limesema linafuatilia kwa karibu tuhuma zilizotolewa na mwananchi mmoja ambaye jina lake linaendelea kufuatiliwa akiwatuhumu askari wawili kupitia mitandao ya kijamii kuwa walimfuata kumtaka afanye nao kazi ya kijajusi pamoja na kumuahidi kumpatia fedha.
Taarifa kwa umma iliyotoleo jana Mei 4,2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania,David Misime imeeleza kuwa Jeshi la Polisi kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai limeunda kikosi kazi ambacho tayari kimeshafika mkoani Mbeya kwa ajili ya uchunguzi juu ya suala hilo.
"Wakati uchunguzi juu ya suala hilo ukiendelea, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi, yeyote mwenye taarifa zitakazosaidia kubaini ukweli juu ya suala hili atoe ushirikiano kwa kutoa taarifa hizo kwa Jeshi la Polisi,"amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED