Rais Samia Suluhu Hassan amewatakia mtihani mwema wanafunzi wa kidato cha sita na Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada, walioanza mitihani yao ya kuhitimu leo Mei 5, 2025.
'Ninawatakia kila la kheri wanangu wote wa Kidato cha Sita na Ualimu ngazi ya Astashahada na Stashahada mnaoanza mitihani yenu ya kuhitimu leo. Hii ni hatua kubwa na muhimu katika safari yenu ya kielimu na kimaisha. Serikali imefanya kazi kubwa kisera na kiuwekezaji katika sekta ya elimu ili muweze kuipata katika mazingira sahihi, na ninaamini mmeandaliwa na kujiandaa vya kutosha kwa mitihani hii.
Mwenyezi Mungu awaongoze na kuwasimamia". ameandika Rais Samia kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED